“Kama ungeweza kufikia japo tone tu la maji safi ya elimu takatifu, ungetambua mara moja kwamba maisha ya ukweli sio maisha ya mwili bali ni maisha ya roho… ”— Bahá'u'lláh

Ufunuo wa Bahá’u’lláh hutuhakikishia kuwa kusudi la maisha yetu ni kumjua Mungu na kufikia uwepo Wake. Asili yetu ya ukweli ni roho zetu zenye utashi, ambazo utashi wake na nguvu zake za uelewa hutuwezesha kuendelea kujiboresha wenyewe na jamii zetu. Kutembea njia ya huduma kwa Mungu na kwa binadamu huyapa maisha maana na hutuandaa kwa ajili ya muda ambao roho hutengana na mwili na huendelea katika safari yake ya milele kuelekea Muumba wake.

Mada nne zinachanganuliwa katika kitengo hiki. Chini ya kila kichwa cha habari, kuna mkusanyiko wa kurasa, makala, na mateuzi kutoka maandiko ya Kibahá’í, na viambatanishi zaidi, ambavyo kuchanganua kila mada kwa undani zaidi.

Roho ya Binadamu »

Kila binadamu ana roho inayodumu milele, yenye utashi ambayo hupita katika dunia hii kwa kipindi kifupi na huendelea milele kuelekea kwa Mungu. Kusudi la maisha yetu ni kuendelea kiroho kwa kuhudumia binadamu wenzetu. Katika kufanya hivyo, tunapata sifa za kiroho ambazo tutazihitaji katika maisha yajayo.

Ibada »

Vitendo vya kuabudu kama sala, tafakari, kufunga, hija, na huduma kwa wengine ni sehemu ya asili ya maisha ya kidini. Kupitia kwavyo, mtu binafsi na jamii wanaweza kuendelea kuimarisha fundo la kipekee kati ya Mungu na binadamu.

Maisha ya Utoaji kwa Ukarimu »

Kama vile kusudi la mshumaa ni kutoa mwanga, roho ya binadamu iliumbwa kutoa kwa ukarimu. Tunafikia kusudi letu la juu kabisa katika maisha ya huduma ambapo, kwa unyenyekevu na kujitenga, tunatoa muda wetu, nguvu, maarifa, na rasilimali fedha.

Sifa na Mienendo »

Uendelezaji wa sifa za kiroho katika dunia hii hautengamani na urekebishaji unaondelea wa mienendo yetu ambapo matendo yetu huendelea kufikia kuakisi ubora na ukamilifu ambao kila mwanadamu amejaliwa nao. Sifa za kiroho kama hizi hazipatikani kwa kukazia katika nafsi; zinaendelezwa katika huduma kwa wengine.