“Kusudi la kimsingi linalohuisha Imani ya Mungu na Dini Yake ni kulinda manufaa na kukuza umoja wa jamii ya binadamu, na kuendeleza roho ya upendo na undugu miongoni wa watu.”— Bahá'u'lláh

Mafanikio ya kanuni ya umoja wa binadamu ni vyote viwili lengo na kanuni ya uendeshaji wa ufunuo wa Bahá’u’lláh. Bahá’u’lláh alifananisha ulimwengu wa binadamu na mwili wa mwanadamu. Katika hiki kiumbe hai, mamilioni ya chembe hai, anuwai katika umbo na shughuli, zinatekeleza kazi zao katika kutunza mfumo wenye afya. Hali kadhalika, uhusiano patanifu miongoni mwa watu binafsi, jumuiya, na asasi zinasaidia kuendeleza jamii na kuruhusu uendeleaji mbele wa ustaarabu.

Mtu Binafsi na Jamii »

Leo tunaishi katika kipindi cha kipekee katika historia. Kadri wanadamu wanavyojitokeza kutoka utoto na kukaribia ukomavu wake wa pamoja, hitaji la uelewa mpya wa mahusiano kati ya mtu binafsi, jumuiya, na asasi za jamii unazidi kuwa wa umuhimu zaidi.

Familia Moja ya Binadamu »

Itikadi kwamba sisi ni wa familia moja ya binadamu ipo kwenye kiini cha Imani ya Kibahá’í. Kanuni ya umoja wa binadamu ni “kile kiini ambapo mafundisho ya Bahá’u’lláh huzungukia…”

Utaratibu wa Kiutawala wa Kibahá’í »

Shughuli za jamii ya Kibahá’í hutawaliwa kupitia mfumo wa asasi, kila moja na uwanja wa utendaji uliowekwa dhahiri. Machimbuko ya mfumo huu, unaojulikana kama Utaratibu wa Utawala, pamoja na kanuni zinazoongoza utendaji wake hupatikana katika Maandiko ya Bahá’u’lláh.