“Hivyo kila mmoja wenu aweze kuwa kama mshumaa unaotoa mwanga wake, kitovu cha mvuto popote watu wanapokuja pamoja; na kutoka kwenu, kama vile kiota cha maua, manukato mazuri yaweze kutoka.” –‘Abdu’l‑Bahá

Maisha ya Utoaji kwa Ukarimu

Kama vile tu kusudi la mshumaa ni kutoa mwanga, roho ya mtu iliumbwa kutoa kwa ukarimu. Tunafikia kusudi letu la juu kabisa katika maisha ya huduma, ambapo tunajitolea muda wetu, nguvu, maarifa, na rasilimali fedha.

Msukumo wa kutoa hutokana na upendo kwa Mungu. Pindi upendo huu hujazapo mioyo yetu, ukarimu huibuka na kubainisha mfumo wa muenendo wetu; wakati tunawahudumia wengine kwa ajili ya upendo wa Mungu, hatusukumwi na tumaini la kujulikana na kuzawadiwa wala kwa hofu ya adhabu. Maisha ya huduma kwa binadamu humaanisha unyenyekevu na kujitenga, sio kujipendelea-nafsi na kutaka kujionesha.

Shoghi Effendi ameandika: “Tunatakiwa tuwe kama mfereji ama chemchemi ambayo huendelea kumwaga vyote ilivyo navyo na huendelea kujazwa kutoka chanzo kisichoonekana. Kuwa wakati wote tukitoa kwa ajili ya mafanikio ya wenzetu bila hofu ya umaskini na kutegemea rehema zisizoshindwa za Chanzo cha utajiri wote na mema yote-hii ndio siri ya kuishi kwa usahihi.


“Kutoa na kuwa mkarimu ni sifa Zangu; kheri ni kwake ambaye amejipamba kwa njema Zangu.”

—  Bahá'u'lláh

{{ note }}: