“Ni kwa mawazo kama haya akilini kwamba Wabahá’í wanaingia katika ushirikiano kwa kadri rasilimali zao zinavyoruhusu, na idadi iongezekayo ya harakati,mashirika, makundi na watu binafsi, wakiunda ubia zinazojitahidi kubadilisha jamii na kusaidia jitihada za umoja, kukuza ustawi wa binadamu,na kuchangia mshikamano wa ulimwengu.”

— Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Bahá’u’lláh aliwashauri wafuasi Wake: “Muwe wenye wasiwasi sana kuhusu mahitaji ya zama ambamo mnaishi, na mlenge majadiliano yenu juu ya dharura zake na mahitaji.

Jinsi ilivyo, Wabahá’í kote duniani—watu binafsi na kwa pamoja—wanajitahidi kushiriki katika maisha ya jamii, wakifanya kazi bega kwa bega na makundi anuwai kuchangia kwenye uendeleaji mbele wa ustaarabu wa kimwili na kiroho.

Maeneo mawili yanayotimizana ya jitihada yanachunguzwa hapa. Shughuli za kijamii huelezea shughuli mbalimbali, zikifanyika mara nyingi kwenye ngazi ya mashina, ambazo kusudi lao ni kuchangia kwenye ustawi wa kimwili na kijamii wa jumuiya pana. Inayohusiana kwa karibu na hii ni jitihada za Wabahá’í kuchangia kwenye ustawi wa umma kwenye ngazi ya fikra kupitia ushiriki katika mijadala ya kijamii. Miongoni mwa wajumbe binafsi wa jumuiya ya Kibahá’í hii kwa kawaida huhusisha kushirikiana mawazo yanayovuviwa na mafundisho ya Kibahá’í katika nyanda za kijamii kadha wa kadha. Mabaraza ya Kiroho ya Kitaifa huratibu jitihada za Kibahá’í kuchangia kwenye mijadala inayozingatia vipengele mbalimbali vya maendeleo ya kijamii, huku kwenye ngazi ya kimataifa, Jumuiya ya Kibahá’í ya Kimataifa inakuwepo katika safu ya mitandao ya kiulimwengu inayohusika na masuala kama vile usawa wa wanaume na wanawake na maendeleo endelevu.

{{ note }}: