“Acha muono wako uwe ukumbatiao ulimwengu mzima…” — Bahá'u'lláh

Katika kipindi chote cha historia, Mungu amekuwa akituma kwa binadamu mfuatano wa Waelimishaji watakatifu—wajulikanao kama Wadhihirishaji wa Mungu—ambao mafundisho yao yametoa msingi kwa ajili ya uendelezaji wa ustaarabu. Wadhihirishaji hawa wamejumuisha Abraham, Krishna, Zoroasta, Musa, Buddha, Yesu Kristo, na Muhammad. Bahá’u’lláh, mtume wa sasa miongoni mwa Mitume hawa, alieleza kuwa dini za ulimwengu huja kutoka Chanzo kimoja na kwa asili ni kurasa zinazofuatana za dini moja kutoka kwa Mungu.

Wabahá'í huamini hitaji muhimu linaloikabili jamii ya binadamu ni kutafuta muono uunganishao wa jamii ya wakati ujao na wa asili na kusudi la maisha. Muono wa namna hiyo hukunjuka katika maandiko ya Bahá'u'lláh.

Kile Wabahá’í Wanachoamini »