“Mungu asifiwe, moyo wako hushughulikia kumbukizi ya Mungu, roho yako hufurahishwa kwa habari njema za Mungu na wewe unazamia sana katika sala. Hali ya sala ni hali bora kabisa…”

— ‘Abdu’l‑Bahá

Huduma na ibada ni sehemu ya kiini cha mpangilio wa maisha ya jumuiya ambayo Wabahá’í kote ulimwenguni wanajaribu kuuleta katika uwepo. Ni vipengele viwili tofauti, lakini vipengele visivyotengana vinavyosogeza mbele maisha ya jumuiya. ‘Abdu’l-Bahá aliandika kwamba, “Mafanikio na ustawi hutegemea juu ya huduma na ibada kwa Mungu”.

Sala ni ya msingi kwa maisha ya Kibahá’í, iwapo kwenye ngazi ya mtu binafsi, jumuiya, au asasi. Wabahá’í hugeuza mioyo yao kwa Mungu mara kwa mara siku nzima—wakisihi msaada Wake, wakimwomba kwa niaba ya wapendwa, wakitoa sifa na shukrani, na wakitafuta thibitisho takatifu na mwongozo. Aidha, mikutano ya mashauriano na mikusanyiko ambamo marafiki wamekuja pamoja kutekeleza mradi mmoja au mwingine mara nyingi huanza na huisha na sala.

Wabahá’í pia wanakaribisha mikusanyiko ambamo marafiki, Wabahá’í na wengine vilevile, wanaungana katika sala, mara nyingi katika nyumba za mmoja kwa mwingine. Mikutano ya ibada kama hii hutumika kuamsha mwelekeo wa kiroho ndani ya washiriki, na pamoja na matendo ya huduma wanayotekeleza, huongoza kwenye muundo wa maisha ya jumuiya unaojawa na roho ya ibada na unaozingatia upatikanaji wa ustawi wa kiroho na kimwili.

Kuunganishwa kwa ibada na huduma hupata kielelezo katika asasi ya Mashriqu’l-Adhkár. Muundo huu hujumuisha jengo la katikati linalokuwa kitovu cha ibada katika eneo la kijiografia, na majengo tegemezi yaliyotengwa kwa ajili ya utoaji wa elimu, huduma za afya na huduma nyingine zinazohusika na maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya jumuiya. Ingawa kuna Mashriqu’l-Adhkár chache tu duniani leo, mbegu za kwa ajili ya kufikia ustawishwaji wake zinaendelea kupandwa katika idadi inayoongezeka ya jumuiya, na huko mbeleni kila kitongoji kitanufaika na majengo kama hayo.

{{ note }}: