“Hitaji la juu kabisa la binadamu ni ushirikiano na kurudishiana fadhila.” –‘Abdu’l‑Bahá

Mtu Binafsi na Jamii

Leo tunaishi katika kipindi cha kipekee katika historia. Kadri wanadamu wanavyojitokeza kutoka utoto na kukaribia ukomavu wake wa pamoja, hitaji la uelewa mpya wa mahusiano kati ya mtu binafsi, jumuiya, na asasi za jamii linakuwa ni la kushinikiza zaidi.

Utegemezi mmoja kwa mwingine wa wahusika hawa watatu katika uendelezaji mbele wa ustaarabu lazima utambuliwe na mifano ya awali ya ugomvi, ambamo kwa mfano, asasi zinashurutisha utii ilhali watu binafsi hupiga kelele wakidai uhuru, inahitaji kubadilishwa na dhana za kina zaidi za majukumu yanayokamilishana yanayopaswa kutekelezwa na kila mmoja katika kujenga ulimwengu bora zaidi.

Kukiri kwamba mtu binafsi, jumuiya, na asasi za jamii ni wahusika wakuu wa ujengaji ustaarabu, na kutenda ipasavyo, hufungua uwezekano kubwa kwa furaha ya binadamu na huruhusu uundaji wa mazingira ambamo uwezo wa kweli wa roho ya binadamu unaweza kuachiwa huru.


“Watu wote wameumbwa kupeleka mbele ustaarabu uendeleao daima.”

— Bahá'u'lláh

{{ note }}: