Kaburi la Báb juu ya Mlima Carmel huko Haifa, Israel — mojawapo ya mahali patakatifu kabisa duniani kwa Wabahá’í.

Báb — Mtangulizi wa Imani ya Kibahá’í

Katikati ya karne ya 19—moja kati ya vipindi vyenye ghasia mno katika histori ya ulimwengu—mfanyabiashara kijana alitangaza kwamba Yeye alikuwa mchukuzi wa ujumbe uliokusudiwa kubadilisha maisha ya binadamu. Kwenye wakati ambapo nchi Yake, Iran, ilikuwa inapitia mmomonyoko mkubwa wa maadili, ujumbe Wake uliamsha msisimko na matumaini miongoni mwa matabaka, ukivutia kwa haraka maelfu ya wafuasi. Alichukua jina “Báb”, linalomaanisha “Lango” katika Kiarabu.

Kwa mwito Wake na marekebisho ya kimaadili, na zingatio Lake la kuboresha nafasi ya wanawake na hali ngumu ya masikini, maagizo ya Báb kwa ufanyaji upya kiroho yalikuwa ya kimapinduzi. Wakati huo huo, alianzisha dini Yake tofauti inayojitegemea, akiwavutia wafuasi Wake kubadilisha maisha yao na kutekeleza matendo makuu ya ujasiri.

Báb alitangaza kwamba jamii ya binadamu ilisimama kwenye kizingiti cha zama mpya. Utume Wake, ambao ulidumu kwa miaka sita tu, ulikuwa kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa Mdhihirishaji wa Mungu Ambaye angeleta zama za Amani na haki, iliyoahidiwa katika dini zote za ulimwengu: Bahá’u’lláh .


“Maisha Yake ni moja ya mifano inayostaajabisha sana ya ujasiri ambayo yamekuwa heshima kubwa kwa binadamu kuyatazama…”

— Taadhima kwa Báb kutoka mwandishi Mfaransa wa karne ya 19, A.L.M Nicolas.

{{ note }}: