“Iwe mbali na utukufu Wake kwamba kalamu ya kibinadamu au ulimi ingedokeza siri Yake…”– Bahá’u’lláh

Ufunuo

Mungu, Muumbaji wa ulimwengu, ni ajuaye yote, mwenye upendo wote na mwenye rehema yote. Kama vile jua la kimwili linavyoangazia dunia, hivyo ndivyo mwanga wa Mungu humiminwa juu ya muumbo wote. Haiwezekani kwa akili yoyote ya kibinadamu kuelewa kiukweli uhalisi wa Mungu. Hata fikra yetu juu ya Mungu iwe pana au bunifu kiasi gani, daima itazuiliwa na mipaka ya akili ya kibinadamu.

Tangu zama za kale, Mungu ametuma Mitume Watakatifu wanaojulikana kama Wadhihirishaji wa Mungu—miongoni mwao Ibrahimu, Krishna, Zoroasta, Musa, Buddha, Yesu Kristo, Muhammad na, hivi karibuni, Báb and Bahá’u’lláh—ili kukuza uwezo wa kiroho, kiakili na kimaadili wa binadamu. Kufuatia ujio wa Mdhihirishaji wa Mungu maendeleo ya ajabu hutokea ulimwenguni. Yakifikia vyanzo vya motisha ya kibinadamu, mafundisho Yake huamsha ndani ya watu wote uwezo kuchangia kwenye uendelezaji wa ustaarabu kwa kiasi ambacho hakikuwezekana awali.

Leo, tunajikuta kwenye kizingiti cha ukomavu wa jamii ya binadamu. Tukipitia hatua mbalimbali, kwa pamoja tumepitia uchanga na utoto. Kote duniani, jamii ya binadamu inaumbwa upya, na mwelekeo wa kimsingi uko wazi: tunashuhudia siyo pungufu kuliko upangaji wa jamii ya binadamu kama ustaarabu wa sayari.


"Tazameni ushahidi wa ajabu wa kazi ya mkono wa Mungu, na tafakarini juu ya wigo wake na tabia."

— Bahá'u'lláh

{{ note }}: