Makao ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu katika kilele cha majengo ya nusu mduara katika Mlima Carmel.

Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ni halmashauri ya kiutawala ya kimataifa ya Imani ya Kibahá’í. Bahá’u’lláh aliamuru kuundwa kwa asasi hii katika kitabu Chake cha sheria, Kitáb-i-Aqdas.

Nyumba ya Haki ya Ulimwengu ni chombo kinachoundwa na wajumbe tisa, ambao huchaguliwa kila miaka mitano na wajumbe wote wa mabaraza ya kitaifa ya Wabahá’í. Bahá’u’lláh alitoa mamlaka takatifu kwa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu kuweka jitihada kuleta mabadiliko chanya kwa uboreshaji wa jamii ya binadamu, kuendeleza elimu, amani na maendeleo ya dunia, na kulinda ubora wa binandamu na nafasi ya dini. Ina wajibu wa kuweka katika vitendo mafundisho ya Kibahá’í kwa mahitaji ya jamii inayoendelea kunyumbulika na hivyo basi imewezeshwa kutunga sheria katika mambo ambayo hayakuelezwa kinagaubaga katika Maandiko Matakatifu ya Imani.

Tangu uchaguzi wake wa mara ya kwanza mnamo1963, Nyumba ya Haki ya Ulimwengu imeiongoza jamii ya Kibahá’í ya ulimwengu katika kujenga uwezo wake kushiriki katika ujengaji wa ustaarabu unaostawi wa ulimwengu. Muongozo unaotolewa na Nyumba ya Haki ya Ulimwengu huhakikisha umoja wa fikra na wa vitendo wa jamii ya Kibahá’í wakati ikijifunza kuweka mtazamo wa Bahá’u’lláh wa amani ya ulimwengu katika vitendo.


“Kama vile kwa kila siku kuna tatizo jipya na kwa kila tatizo kuna ufumbuzi unaofaa, mambo kama hayo yanapaswa yapelekwe kwa Wachungaji wa Nyumba ya Haki ili waweze kutenda kufuatana na mahitahi na haja za wakati.”

— Bahá’u’lláh

{{ note }}: