“Muwe kama vidole vya mkono mmoja, na viungo vya mwili mmoja. Hivyo ndivyo iwashauriavyo Kalamu ya Ufunuo…” – Bahá’u’lláh

Familia Moja ya Binadamu

Itikadi kwamba sisi ni wa familia moja ya binadamu ipo katika kiini cha Imani ya Kibahá’í. Kanuni ya umoja wa binadamu ni “kile kiini ambapo mafundisho ya Bahá’u’lláh huzungukia”.

Bahá’u’lláh alifananisha ulimwengu wa binadamu na mwili wa mwanadamu. Katika hiki kiumbe hai, mamilioni ya chembe hai, anuwai katika umbo na shughuli, zinatekeleza kazi zao katika kutunza mfumo wenye afya. Kanuni inayotawala kazi za mwili ni ushirikiano. Sehemu zake mbalimbali hazishindanii rasilimali, bali, kila chembe-hai, kutoka mwanzo wake, huunganishwa na mchakato endelevu wa kutoa na kupokea.

Kukubali umoja wa binadamu huhitaji kwamba hisia za chuki au upendo usio na sababu—iwe ya rangi, dini, au kuhusiana na jinsia—lazima iondolewe kabisa.


“Kuna undugu kamili kama msingi wa binadamu, kwa kuwa wote ni watumishi wa Mungu mmoja na ni wa familia moja chini ya ulinzi wa majaaliwa matakatifu.”

— ‘Abdu’l‑Bahá

{{ note }}: