“Njia ya maisha ni barabara ambayo hupelekea kwenye maarifa na mafanikio ya kiroho” –‘Abdu’l‑Bahá

Roho ya Binadamu

Utambulisho wa kimsingi wa kila binadamu ni roho yenye uwezo wa kufikiri kimantiki na inayodumu milele, ambayo iko“nje kabisa ya utaratibu wa muumbo wa kimwili. Bahá’u’lláh hutumia mfano wa jua kuelezea uhusiano kati ya roho na mwili: “Roho ya mtu ni jua ambalo kwalo mwili wake huangaziwa, na kutoka kwake hupata riziki yake, na inapaswa kuangaliwa namna hiyo.

Ni kupitia matumizi ya nguvu za roho ambapo mafanikio ya binadamu hupatikana. ‘Abdu’l-Bahá alisema kuhusu roho “ huweza kugundua uhalisia wa vitu, kuelewa upekee wa viumbe, na kupenya katika fumbo la uwepo. Sayansi zote, maarifa, sanaa, maajabu, asasi, ugunduzi na shughuli za biashara huja kutokana na kutumia akili ya roho yenye uwezo wa kufikiri.

Tunaweza kuakisi sifa za kiroho kwa kiwango ambacho tunasafisha vioo vya roho na fikra zetu kupitia sala, usomaji na uwekaji kwa vitendo wa Maandiko Matakatifu, upataji wa maarifa, jitihada za kuboresha mienendo yetu na kushinda majaribio na shida, na huduma kwa binadamu.

Wakati kifo hutokea katika dunia hii, roho hutenganishwa na mwili, na huendelea katika safari isiyo na kikomo kuelekea ukamilifu.


“Pale ambapo roho ina uhai mtakatifu ndani mwake, hapo ndipo huleta tunda zuri na hugeuka kuwa mti wa mbinguni.”

— ‘Abdu’l‑Bahá

{{ note }}: