‘Abdu’l‑Bahá, Mkuu wa Imani ya Kibahá’í baada ya kupaa kwa Bahá’u’lláh.

‘Abdu’l‑Bahá — Kielelezo Kamili

Mnamo miaka ya mwanzo ya karne ya 20, ‘Abdu’l-Bahá—Mwanae mkubwa kabisa wa kiume wa Bahá’u’lláh—alikuwa mtetezi mkuu wa Imani ya Kibahá’í, maarufu kama bingwa wa haki ya kijamii na balozi kwa ajili ya amani ya kimataifa.

‘Abdu’l-Bahá (1844-1921)

Akisimamia umoja kama kanuni ya msingi ya mafundisho Yake, Bahá’u’lláh alianzisha kinga ihitajikayo kuhakikisha kuwa dini Yake katu isingefuata mkondo wa zile zingine ambazo ziligawanyika katika madhehebu baada ya kifo cha Waanzilishi wao. Katika Maandiko Yake, Yeye aliwaagiza wote kumgeukia Mwanaye Mkubwa wa Kiume, ‘Abdu’l-Bahá, siyo tu kama mfasiri mwenye mamlaka wa Maandiko ya Kibahá’í bali pia kama mfano kamili wa roho ya Imani hii na mafundisho.

Baada ya kupaa kwa Bahá’u’lláh, sifa za tabia zisizo za kawaida za ‘Abdu’l-Bahá, ujuzi Wake na utumishi Wake kwa jamii ya binadamu vilitoa picha dhahiri ya mafundisho ya Bahá’u’lláh katika vitendo, na vilileta heshima kubwa kwa jumuiya iliyokuwa ikipanuka kwa haraka kote ulimwenguni.

‘Abdu’l-Bahá aliweka wakfu uchungaji Wake katika kupeleka mbele Imani ya Baba Yake na kuendeleza mawazo ya amani na umoja. Alihamasisha uanzishwaji wa asasi za Kibahá’í za mahali, na aliongoza miradi michanga ya kielimu, kijamii na kiuchumi. Baada ya kuachiliwa Kwake kutoka kifungo cha maisha, ‘Abdu’l-Bahá alifanya mfululizo wa ziara ambazo zilimpeleka Misri, Ulaya na Amerika ya Kaskazini. Katika maisha Yake yote, Yeye aliwasilisha kwa lugha nyepesi na kwa ufasaha, kwa wakubwa na wadogo kadhalika, dawa ya Bahá’u’lláh kwa ajili ya urejesho wa kiroho na kijamii wa jamii.


Yeyote aliyeshirikiana Naye amemuona ndani Mwake mtu mwenye ujuzi wa kupita kiasi, Ambaye lugha Yake inavutia, Ambaye anavutia akili na roho, Ambaye amejitolea kwa ajili ya itikadi katika umoja wa wanadamu…

— Gazeti laAl-Mu’ayyad, Misri, 16 Oktoba 1910

{{ note }}: