“Watu wote wameumbwa kupeleka mbele ustaarabu uendeleao daima.” – Bahá’u’lláh

Ustaarabu Unaoendelea Mbele Daima

Binadamu, maandiko ya Kibahá’í hueleza, wamepita hatua ya utoto na sasa husimama kwenye kizingiti cha ukomavu wake wa pamoja. Mabadiliko ya kimapinduzi na yanayofikia mbali ambayo yanatokea leo ni sehemu muhimu ya kipindi hiki cha mapito—wakati ambao huweza kufananishwa na ujana. Katika kipindi hiki, fikira, mitazamo, na mazoea kutoka hatua za awali za binadamu vinafagiliwa mbali na mielekeo mipya ya fikira na utendaji vinavyoakisi ukomavu unaokaribia vinaanza kushika mizizi. ‘Abdu’l-Bahá anaeleza: “Kile ambacho kilikuwa chenye manufaa kwa mahitaji ya mwanadamu wakati wa historia ya mwanzo ya mbari hii hakiwezi kuridhisha wala kutosheleza mahitaji ya siku hii, kipindi hiki cha upya na cha ukamilisho.” Anaendelea: “Mwanadamu anapaswa sasa kuwa aliyejawa na njema mpya na nguvu, viwango vipya vya kimaadili, uwezo mpya…Vipaji na baraka za kipindi cha ujana, ingawa ni vya wakati muafaka na kutosheleza enzi za ujana wa binadamu, sasa haviwezi kukidhi mahitaji ya ukomavu wake.

Sifa bainifu ya umri wa ukomavu huu unaokaribia ni kuunganishwa kwa jamii ya binadamu. Shoghi Effendi anaandika kwamba, ingawa umoja “wa familia, wa kabila, wa mji-jimbo, na taifa umejaribiwa kwa msururu na kuwekwa imara” umoja unaokumbatia ulimwengu ni “lengo ambalo kwalo binadamu waliohangaishwa wanajitahidi kulifikia.” Katika kifungu kingine, anarejea kwenye “uzinduzi wa ustaarabu wa kiulimwengu wa kiasi kwamba hakuna jicho la kiuanadamu ambalo limewahi kuuona au akili ya kibinadamu kuufikiria.” Anauliza: “Nani anaweza kuwaza kiwango cha juu sana ambacho ustaarabu wa namna hiyo, jinsi unavyojikunjua wenyewe, umekusudiwa kukifikia? Nani anaweza kupima kimo ambazo akili ya binadamu, ikiwa huru kutoka pingu zake, itapaa? Nani anaweza kupata sura ya falme ambazo roho ya binadamu, iliyojazwa na nguvu kupitia mwanga umiminiwao wa Bahá’u’lláh, uking’ara katika ukamilifu wa utukufu wake, itagundua?

Kuibuka kwa ustaarabu wa ulimwengu wenye usitawi katika mielekeo yake yote miwili ya kiroho na ya kimwili humaanisha kwamba vipengele vya kiroho na vya kiutendaji vya maisha vinasogea mbele pamoja. Kupitia imani na mantiki, inawezekana kugundua nguvu na uwezo vinavyofichwa ndani ya watu binafsi na binadamu kwa jumla, na kufanya kazi kupata uwezekano huu. Utambuzi wa mapatano ya kimsingi kati ya sayansi na dini pia huruhusu uzalishaji, utumiaji, na uenezaji wa ujuzi wa kiroho na kimwili miongoni mwa wakazi wa dunia.


“Ustawi wa binadamu, amani na usalama wake, haviwezi kupatikana isipokuwa na mpaka tu umoja wake umewekwa imara.”

— Bahá'u'lláh

{{ note }}: