“Matunda ya mti wa mtu daima yamekuwa na ni vitendo vyema na tabia za kusifiwa.” –Bahá’u’lláh

Sifa na Mienendo

Cha msingi katika maisha ya kiroho ni ukuzaji wa sifa za kiroho ambazo hutusaidia kila mmoja wetu katika safari yetu ya milele kuelekea kwa Mungu. Katika dunia hii, uendelezaji wa sifa kama hizo hautengamani na uboreshaji unaondelea wa mienendo yetu ambapo vitendo vyetu kwa idadi iongezekayo hufikia kuakisi ubora na ukamilifu (uadilifu) ambavyo kila binadamu amejaliwa navyo. ‘Abdu’l-Bahá husema:

Tunatakiwa kuweka jitihada bila kukoma na bila kupumzika kufanikisha ukuzaji wa asili ya kiroho ya mtu, na kuweka jitihada kwa nguvu zisizochoka kuendeleza jamii ya binadamu kuelekea ubora wa ukweli na uliokusudiwa wa daraja lake.

Sifa za kiroho huendelezwa katika mazingira ya upendo na maarifa yanayokua, na kulingana na sheria za kiroho. Jinsi tunavyoruhusu maarifa ya Mungu kuongezeka katika fikra na mioyo yetu, sifa za asili yetu ya juu huanza kuendelea. Kwa uelewa unaoongezeka na kuongezeka, tunaweza kutenganisha kati ya kile kinachofaa ufahari na kile ambacho kinapelekea mshuko, na tunaendelea katika uelewa wetu wa ulimwengu uliotuzunguka, binadamu, jamii na maisha ya roho. Upendo huongezeka na maarifa na uelewa wa ukweli huwezeshwa na upendo. Uwili usiofaa kati ya moyo na fikra huepukwa.

Kuna vitu vingi ambavyo huchangia katika maendeleo haya, kati yao sala, tafakari, utayari kujifunza, na jitihada za kila siku—haswa katika huduma kwa jamii ya binadamu. Katika jitihada ya kuishi maisha ya kiroho, kukazia sana katika nafsi kunaweza kuwa na matokeo kinyume. Bahá’u’lláh huandika kwamba inatupasa kukazia mawazo yetu katika “kile ambacho kitatakasa…mioyo na roho za binadamu.” “Hii,” Huendelea, “inaweza kupatikana kupitia matendo safi na mema, kupitia maisha mema na tabia nzuri.” ‘Abdu’l-Bahá ameandika: “Jinsi gani alivyo bora, jinsi gani alivyo wa kusifiwa mtu ambaye huinuka kutimiza wajibu wake; jinsi gani alivyo asiye thamani na wakutia aibu, kama akifumba macho yake kutoka ubora wa jamii na kupoteza maisha yake yenye thamani akifukuzia maslahi binafsi na manufaa yake mwenyewe.

Tunaweza kufikiria jitihada zetu kuendeleza sifa za kiroho kama vile kutembea kwa unyenyekevu na Bwana wetu, tukikazana na tukijifunza, tukijitenga na hisia za hatia, tukikubaliana na ufanyaji makosa usioepukika, lakini bila kupoteza mkazo wa kile ambacho kwa asili kimo ndani mwetu. Ingawa ugumu na kurudi nyuma ni vitu visivyokwepeka, hii ni jitihada ya shangwe, iliyojaa furaha tele.

Kati ya hatari kubwa katika mchakato wa maisha haya yote, katika uboreshaji wa mienendo unaenda kwa utaratibu, ni kujiona tu wakamilifu, kujiona tu bora kuliko wengine na majivuno—mienendo ambayo huharibu kabisa jitihada zote za kiroho na kuangusha msingi wake. Bahá’u’lláh ameandika:

“ENYI WANADAMU! Hamjui kwa nini tuliwaumba ninyi wote kutokana na mavumbi yale yale? Ili asiweko yeyote wa kujitukuza juu ya mwingine. Fikirini wakati wote mioyoni mwenu jinsi mlivyoumbwa. Kwa kuwa tumewaumba ninyi nyote kutokana na kitu kile kile kimoja mnapaswa kuwa hata kama roho moja, kutembea na miguu ile ile, kula kwa mdomo ule ule na kuishi katika nchi moja, ili kutoka katika nafsi yenu ya ndani kabisa, kwa vitendo vyenu na kazi zenu, ishara za umoja wenu na kiini cha kujitenga vipate kudhihirika. Hili ndilo shauri Langu kwenu, enyi jeshi la mwangaza! Lisikieni shauri hili ili muweze kulipata tunda la utakatifu kutoka katika mti wa utukufu wa ajabu.”


Kulingana na asili ya mada ambayo imeangaliwa, mkusanyiko wa mada hii umechukua utaratibu tofauti na ile mingine katika tovuti hii. Inajumuisha makala moja kuhusu sheria za kiroho, ikifuatwa na mateuzi toka Maandiko ya Imani ya Kibahá’í yaliyopangwa katika mada nne; upendo na maarifa; ukweli, uaminifu, na haki; usafi wa moyo; na unyenyekevu na kuweka imani katika Mungu. Kama ilivyo katika mijumuisho ya mada zingine, hata hivyo, baadhi ya makala na rasilimali husika zimejumuishwa.

{{ note }}: