“Ikiwa upendo na makubaliano ni dhahiri katika familia moja, familia hii itaendelea mbele, kuwa iliyotiwa mwanga na ya kiroho…”

— ‘Abdu’l‑Bahá

Nguzo ya familia ni kitovu cha jamii ya binadamu. Hutoa mazingira muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya sifa zinazostahili kutukuzwa na uwezo. Kupitia utendaji wake linganifu na ustawishwaji na utunzwaji wa vifungo vya upendo unaounganisha pamoja wajumbe wake, hutoa kielelezo kidumucho kwenye ukweli kwamba ustawi wa mtu binafsi hufungamana kabisa na maendeleo na ustawi wa wengine.

Dhima ya msingi ya familia ni kulea watoto ambao wanaweza kuchukua madaraka kwa vyote viwili ukuaji wao wa kiroho na ushiriki wao katika uendelezaji mbele wa ustaarabu. ‘Abdu’l-Bahá anasema kwamba mama na baba wa mtoto wanapaswa “kama wajibu…kujitahidi kwa juhudi zote kuwafunza binti na mwana”, na wazazi Wabahá’í, ambao hubeba majukumu ya kwanza kwa malezi ya watoto wao, wawe zingatifu wa wajibu wao husika. Lakini elimu ya watoto siyo tu jukumu la wazazi. Jumuiya pia ina jukumu muhimu la kutekeleza na jumuiya ya Kibahá’í hutia mkazo mkubwa kwenye mada hii. Bila shaka, madarasa, yaliyo wazi kwa wote, kwa ajili ya elimu ya kiroho na kimaadili ya watoto, ni mfano mzuri miongoni mwa shughuli za awali zinazoshughulikiwa na Wabahá’í katika mahali.

{{ note }}: