Acha muono wako uwe ukumbatiao ulimwengu mzima
— Bahá’u’lláh
Katika kipindi chote cha historia, Mungu amekuwa akituma kwa binadamu mfuatano wa Waelimishaji watakatifu—wajulikanao kama Wadhihirishaji wa Mungu—ambao mafundisho yao yametoa msingi kwa ajili ya uendelezaji wa ustaarabu. Wadhihirishaji hawa wamejumuisha Abraham, Krishna, Zoroasta, Musa, Buddha, Yesu Kristo, na Muhammad. Bahá’u’lláh, mtume wa sasa miongoni mwa Mitume hawa, alieleza kuwa dini za ulimwengu huja kutoka Chanzo kimoja na kwa asili ni kurasa zinazofuatana za dini moja kutoka kwa Mungu.
Wabahá'í huamini hitaji muhimu linaloikabili jamii ya binadamu ni kutafuta muono uunganishao wa jamii ya wakati ujao na wa asili na kusudi la maisha. Muono wa namna hiyo hukunjuka katika maandiko ya Bahá’u’lláh.
Uchunguzaji wa Maeneo ya Dhima
Chunguza chini mateuzi kutoka dhima zilizo katika kiini cha imani na matendo ya Kibahá’í.
Kama wasomi na watu wenye busara wa ulimwengu wa kipindi hiki wangeruhusu binadamu kuvuta manukato ya urafiki na upendo, kila moyo unaoelewa ungeelewa maana ya uhuru wa kweli, na kugundua siri ya amani isiyovurugika na utulivu kabisa.
– Bahá’u’lláh –
Maktaba ya Kibahá’í ya Marejeo
Maktaba ya Kibahá’í ya Marejeo ni chanzo cha kimamlaka cha mtandaoni cha maandiko ya Kibahá’í.
Tembelea MaktabaNi pamoja na mawazo kama haya akilini kwamba Wabahá’í huingia kwenye ushirikiano, kadiri rasilimali zao zinavyoruhusu, kwa idadi iongezekayo ya mijongeo, mashirika, makundi na watu binafsi, kuanzisha ushirikiano ambao unajitahidi kuibadilisha jamii na kuendeleza mbele hoja ya umoja, kukuza ustawi wa binadamu, na kuchangia mshikamano wa ulimwengu.
– Nyumba ya Haki ya Ulimwengu –
Jumuiya ya Ulimwengu
Imani ya Kibahá’í imeanzishwa katika zaidi ya maeneo 100,000 takribani katika kila nchi na majimbo kote ulimwenguni. Hapa chini unaweza kuona viunganishi kwa tovuti za jumuiya nyingi za Kibahá’í za Kitaifa.
Tembelea Tovuti za Kitaifa za Kibahá’í