Imani Ya Kibahá’í

Tovuti ya jumuiya ya Kibahá’í ya kiulimwengu

Imani Ya Kibahá’í

Kile Wabahá’í Wanachoamini

Maelezo ya jumla

Katika maelfu kwa maelfu ya maeneo kote ulimwenguni, mafundisho ya Imani ya Kibahá’í yanawavutia watu binafsi na jumuiya wanapojitahidi kuboresha maisha yao wenyewe na kuchangia kwenye uendelezaji wa ustaarabu. Itikadi za Kibahá’í hushughulikia mada muhimu sana kama vile umoja wa Mungu na dini, umoja wa binadamu na uhuru kutokana na chuki au mapenzi yasiyo na sababu, asili bora ya mwanadamu, ufunuo uendeleao wa ukweli wa kidini, ukuzaji wa sifa za kiroho, muungano wa ibada na huduma, usawa wa kimsingi wa jinsi, upatano kati ya dini na sayansi, umuhimu mkuu wa haki katika jitihada zote za kibinadamu, umuhimu wa elimu, na mienendo ya uhusiano ambao utawaunganisha pamoja watu binafsi, jumuiya, na asasi, kadri jamii ya binadamu isongavyo mbele kuelekea ukomavu wake wa pamoja.

Yeye Ambaye ni Bwana wenu, Mwenye-Rehema Zote, huthamini moyoni Mwake shauku ya kuona mbari nzima ya binadamu kama roho moja na mwili mmoja.
Bahá’u’lláh

Uchunguzaji wa Maeneo ya Dhima

Eneo hili la tovuti linalenga kupanga baadhi ya imani kuu za Kibahá’í kwenye maeneo kadhaa ya dhima.

Maktaba ya Kibahá’í ya Marejeo

Ili kupata utambuzi kamili wa itikadi za Kibahá’í huenda utataka kutembelea Maktaba ya Kibahá’í ya Marejeo ambako unaweza kusoma Maandiko ya Báb, Bahá’u’lláh, na ‘Abdu’l-Bahá pamoja na juzuu zilizoandikwa na Shoghi Effendi na teuzi la matamko na mawasiliano ya Nyumba ya Haki ya Ulimwengu.

Tembelea Maktaba

Enyi wanaadamu! Kusudi la kimsingi linalohuisha Imani ya Mungu na Dini Yake ni kulinda manufaa na kukuza umoja wa jamii ya binadamu, na kuendeleza roho ya upendo na undugu miongoni mwa watu…Chochote kinachojengwa juu ya msingi huu, mabadiliko na mikasa ya dunia hayawezi kudhoofisha nguvu zake, wala mageuzi ya karne zisizohesabika hayawezi kuyumbisha muundo wake.

Bahá’u’lláh

Kile Wabahá’í Wanachoamini