Imani Ya Kibahá’í

Tovuti ya jumuiya ya Kibahá’í ya kiulimwengu

Kile Wabahá’í Wanachoamini

Maisha ya Utoaji kwa Ukarimu

Utangulizi

Kama vile kusudi la mshumaa ni kutoa mwanga, roho ya binadamu iliumbwa kutoa kwa ukarimu. Tunafikia kusudi letu la juu kabisa katika maisha ya huduma ambapo, kwa unyenyekevu na kujitenga, tunatoa muda wetu, nguvu, maarifa, na rasilimali fedha.

Msukumo wa kutoa hutokana na upendo kwa Mungu. Pindi upendo huu hujazapo mioyo yetu, ukarimu huibuka na kubainisha mfumo wa muenendo wetu; wakati tunawahudumia wengine kwa ajili ya upendo wa Mungu, hatusukumwi na tumaini la kujulikana na kuzawadiwa wala kwa hofu ya adhabu. Maisha ya huduma kwa binadamu humaanisha unyenyekevu na kujitenga, sio kujipendelea-nafsi na kutaka kujionesha.

Shoghi Effendi ameandika: “Tunatakiwa tuwe kama mfereji ama chemchemi ambayo huendelea kumwaga vyote ilivyo navyo na huendelea kujazwa kutoka chanzo kisichoonekana. Kuwa wakati wote tukitoa kwa ajili ya mafanikio ya wenzetu bila hofu ya umaskini na kutegemea rehema zisizoshindwa za Chanzo cha utajiri wote na mema yote-hii ndio siri ya kuishi kwa usahihi.”

Kutoa na kuwa mkarimu ni sifa Zangu; kheri ni kwake ambaye amejipamba kwa njema Zangu.
Bahá’u’lláh

Uchunguzaji wa mada hii

Mkusanyo huu wa kurasa unachunguza mafundisho ya Kibahá’í kuhusu maisha ya kutoa kwa ukarimu. Sehemu ya makala na rasilimali inajumuisha nyenzo zinazotoa uchunguzi wa kina zaidi wa mada hii.