Kile Wabahá’í Wanachoamini
Familia Moja ya Binadamu
Utangulizi
- Kile Wabahá’í Wanachoamini
- Maelezo ya jumla
- Bahá’u’lláh na Ahadi Yake
- Maisha ya roho
- Mungu na Muumbo Wake
- Mahusiano ya Kimsingi
- Amani ya Ulimwengu
- Kile Wabahá’í wanachofanya
Itikadi kwamba sisi ni wa familia moja ya binadamu ipo katika kiini cha Imani ya Kibahá’í. Kanuni ya umoja wa binadamu ni “kile kiini ambapo mafundisho ya Bahá’u’lláh huzungukia”.
Bahá’u’lláh alifananisha ulimwengu wa binadamu na mwili wa mwanadamu. Katika hiki kiumbe hai, mamilioni ya chembe hai, anuwai katika umbo na shughuli, zinatekeleza kazi zao katika kutunza mfumo wenye afya. Kanuni inayotawala kazi za mwili ni ushirikiano. Sehemu zake mbalimbali hazishindanii rasilimali, bali, kila chembe-hai, kutoka mwanzo wake, huunganishwa na mchakato endelevu wa kutoa na kupokea.
Kukubali umoja wa binadamu huhitaji kwamba hisia za chuki au upendo usio na sababu—iwe ya rangi, dini, au kuhusiana na jinsia—lazima iondolewe kabisa.
Muwe kama vidole vya mkono mmoja, viungo vya mwili mmoja. Hivi ndivyo Kalamu ya Ufunuo inavyowashauri…







