Imani Ya Kibahá’í

Tovuti ya jumuiya ya Kibahá’í ya kiulimwengu

Kile Wabahá’í Wanachoamini

Mtu Binafsi na Jamii

Utangulizi

Leo tunaishi katika kipindi cha kipekee katika historia. Kadri wanadamu wanavyojitokeza kutoka utoto na kukaribia ukomavu wake wa pamoja, hitaji la uelewa mpya wa mahusiano kati ya mtu binafsi, jumuiya, na asasi za jamii unazidi kuwa wa umuhimu zaidi.

Utegemezi mmoja kwa mwingine wa wahusika hawa watatu katika uendelezaji mbele wa ustaarabu lazima utambuliwe na mifano ya awali ya ugomvi, ambamo kwa mfano, asasi zinashurutisha utii ilhali watu binafsi hupiga kelele wakidai uhuru, inahitaji kubadilishwa na dhana za kina zaidi za majukumu yanayokamilishana yanayopaswa kutekelezwa na kila mmoja katika kujenga ulimwengu bora zaidi.

Kukiri kwamba mtu binafsi, jumuiya, na asasi za jamii ni wahusika wakuu wa ujengaji ustaarabu, na kutenda ipasavyo, hufungua uwezekano kubwa kwa furaha ya binadamu na huruhusu uundaji wa mazingira ambamo uwezo wa kweli wa roho ya binadamu unaweza kuachiwa huru.

Watu wote wameumbwa kupeleka mbele ustaarabu uendeleao daima.
Bahá’u’lláh

Uchunguzaji wa mada hii

Mkusanyo huu wa kurasa unachunguza zaidi mada ya mtu binafsi na jamii.