Imani Ya Kibahá’í

Tovuti ya jumuiya ya Kibahá’í ya kiulimwengu

Kile Wabahá’í Wanachoamini

Ibada

Utangulizi

Vitendo vya ibada ni kawaida kwa maisha ya kidini. Kupitia humo, watu binafsi na jumuiya wakati wote huendelea kuimarisha fundo la kipekee lililopo kati ya Mungu na jamii ya wanadamu. Fundo hili huhuisha mahusiano yanayosarifu jamii—kati ya watu binafsi na miongoni mwa vipengele tofauti vya jumuiya na asasi zake.

Ibada ni ya lazima kwa ajili ya chakula chetu cha kiroho na ukuaji. Kupitia humo sisi tunaweza kumsifu Mungu na kueleza upendo wetu kwa ajili ya Yake, pia tunaweza kumsihi kupata msaada Wake. Uwezo wa kutafakari ni kipengele kinachobaini mwanadamu. Kwa uhakika, maandiko ya Ki-Bahá’í yanapendekeza kuwa maendeleo wa wanadamu yasingewezekana bila tafakuri na kufikiri. Kufunga saumu na kuhiji ni vitendo vingine viwili vya ibada ambavyo vimekuwa na nafasi muhimu katika maisha ya kidini kupitia historia nzima ya wanadamu. Kazi pia inaweza kuwa tendo la ibada pale inapofanywa katika roho ya utumishi.

Kusanyikeni pamoja kwa furaha na urafiki wa hali ya juu kabisa na someni aya zilizofunuliwa na Bwana mwenye rehema. Kwa kufanya hivyo milango ya maarifa ya kweli itafunguliwa katika nafsi zenu, na hapo mtahisi roho zenu zimejaaliwa uimara na mioyo yenu imejaa furaha angavu.
Bahá’u’lláh

Uchunguzaji wa mada hii

Mkusanyo huu wa kurasa unachunguza mafundisho ya Kibahá’í kuhusu sala, kutafakari na kufunga.