Imani Ya Kibahá’í

Tovuti ya jumuiya ya Kibahá’í ya kiulimwengu

Kuchomoza kwa Mwanga

Miaka mia mbili iliyopita, Báb alitokea, kuanzisha Kipindi kipya na kuandaa ulimwengu kwa mwangaza wa Ufunuo wa Bahá’u’lláh.

Kuchomoza kwa Mwanga huonyesha watu binafsi kadhaa kutoka mabara tofauti ulimwenguni wakielezea utafutaji wao binafsi wa ukweli na kusudi maishani. Wanashiriki ugunduzi wao kuwa Mungu amewatuma Waadhihirishaji Watakatifu wawili—Báb na Bahá’u’lláh—mafundisho Yao yanaleta mapinduzi na mabadiliko ya fikra na tabia za kibinadamu, yakibadilisha giza kuwa mwanga. Filamu inaonyesha ishara za ugunduzi huu zikihamasisha jitihada za wengi ulimwenguni kote kutoa huduma kwa ulimwengu na kuchangia katika ujenzi wa aina mpya ya mtindo wa maisha.

Before downloading please refer to the Terms of use