Imani Ya Kibahá’í

Tovuti ya jumuiya ya Kibahá’í ya kiulimwengu

Kile Wabahá’í wanachofanya

Vijana

Nyenzo kutoka kwenye makongamano ya vijana

Kipindi cha Ujana

Kundi la vijana saba wakiimba pamoja

Miongoni mwa mada zilizochunguzwa wakati wa mfululizo wa makongamano ya vijana yaliyofanyika duniani kote mwaka 2013 na mawimbi ya mikusanyiko iliyofuata, moja ilikuwa mahsusi ikihusu uwezo na tabia zinazohusishwa na kipindi cha ujana.

Aya zifuatazo zimenukuliwa kutoka kwenye nyenzo zilizosomewa na washiriki wa makongamano kuhusu mada hii.

Makongamano ya vijana hukusanya vijana wa rika na uzoefu mbalimbali. Wengi ni vijana balehe ambao, kupitia shule, familia, na maisha ya jumuiya, wanajiandaa kwa majukumu ya utu uzima. Wengine ni vijana wakubwa ambao huenda wako chuoni au wanafanya kazi, wameoa/kuolewa au wako katika mchakato wa kuanzisha familia. Kwa baadhi yao, hali za kijamii zimewalazimisha kubeba majukumu ya watu wazima zaidi, na ustawi wa familia zao tayari unategemea wao. Kadhalika, jamii wanazotokea ni tofauti sana, kuanzia vijiji vidogo vya dunia hadi vitongoji vya miji mikubwa yenye mamilioni ya wakazi.

Bila kujali hali zao za kijamii, vijana hutamani kukua kiroho na kiakili na “kuchangia kwenye ustawi wa binadamu”. Wana nguvu nyingi nzuri, na kuzitumia ipasavyo ni jambo la msingi, kwani zikipotoshwa au kutumiwa vibaya na wengine, zinaweza kusababisha madhila mengi kijamii. Miongoni mwa vijana wa dunia wako wale walio hai kwa maono ya Bahá’u’lláh ya ulimwengu wenye ustawi wa kiroho na kimwili.

Katika huduma isiyo na ubinafsi kwa jamii ndipo kuna fursa ya ukuaji binafsi na kukuza uwezo wa kuchangia kwenye maendeleo ya kijamii. “Kuhudumia binadamu ni kuhudumia Mungu,” ‘Abdu’l-Bahá amesisitiza. Kwa kuelekeza vipaji na uwezo wao kwenye kuinua jamii, “wanakuwa sababu ya utulivu wa ulimwengu wa uumbaji”. Wanapojaa roho ya ukarimu katika shughuli zao za kila siku na kutoa huduma kwa hiari kwa ajili ya ustawi wa wengine, huvutia msaada na thibitisho za Mungu.

Ni muhimu basi kwamba idadi inayoongezeka ya wale walio kwenye kilele cha maisha yao “wajiimarishe kwa ajili ya maisha ya huduma” kwa jamii. Ni kweli mambo mengi huwajaza muda na nguvu: elimu, kazi, burudani, maisha ya kiroho, afya ya mwili. Lakini hujifunza kuepuka mtazamo wa maisha usio na uhusiano baina ya vipengele mbalimbali vya maisha. Mtazamo huu usiolingana mara nyingi humfanya mtu kuwa mwathirika wa uchaguzi potofu unaosukumwa na maswali kama vile; je, mtu asome au ahudumu, apige hatua kimwili au achangie ustawi wa wengine, afanye kazi au ajitoe kikamilifu kwa huduma. Kukosa kuangalia maisha kama kitu kimoja kizima kunaleta wasiwasi na kuchanganyikiwa. Kupitia huduma, vijana hujifunza kukuza maisha ambapo vipengele vyake hutimizana.

Wakiwa na uhakika wa baraka zisizokoma za Mungu kwa wale wanaoinuka kuhudumia, vijana hutazama mazingira wanayoshirikiana na wengine—familia, kundi la marafiki, shule, mahali pa kazi, vyombo vya habari, jumuiya—na kutambua nguvu za kijamii zinazotawala ndani yake. Baadhi ya nguvu hizi, kama vile upendo wa ukweli, kiu ya maarifa, na kuvutiwa na uzuri, huwasukuma katika maendeleo yao kwenye njia ya huduma. Nyingine, kwa mfano mizizi ya mali na kujipendelea, ni mbovu na kwa kupotosha mtazamo wa vijana kuhusu dunia huzuia ukuaji binafsi na wa pamoja. Wanavyoendelea katika jitihada zao za kuchangia ujenzi wa dunia bora, uwezo wao wa kuitumia nguvu za kiroho na kijamii zinazowafanya wajenzi wa ustaarabu huongezeka mara nyingi zaidi.

Maswali ya tafakari

Ni nguvu gani chanya au hasi zinazotawala katika mazingira ambayo vijana huingiliana? Ni kwa njia gani maeneo haya yanaweza kuathiri vijana?

Unaona jukumu gani la kizazi chako katika jamii? Ni lengo gani la juu linaongoza vitendo vyako binafsi na vya pamoja?

Zungumzia athari chanya ambayo huduma inayo kwa maendeleo ya kiroho na kiakili na juu ya uwezo wa kizazi cha vijana kuchangia maendeleo ya kijamii.

Youth drawing sketch of neighbourhood.
Dozen of people consulting together.
Large group of youth watching something attentively.
Four youth laughing together.
Group of youth reflecting in joy.
Large group of youth studying material together.
A group of young people walking among the greenery.

Chunguza nyenzo kutoka kwenye makongamano ya vijana

Unaweza kusoma zaidi kuhusu mada hii katika makala zifuatazo.